TANESCO yakabidhiwa dhamana ya Shilingi Trilioni 1.7

0
304

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) limekabidhiwa dhamana ya Shilingi Trilioni 1.7 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji – Stigler’s Gorge.

Dhamana hiyo iliyotolewa na Benki ya CRDB na UBA, ni kwa ajili ya malipo ya kwanza ambayo ni kinga endapo Mkandarasi anayetekeleza mradi huo atashindwa kutekeleza majukumu yake.