TANESCO SACCOS yakabidhi shuka 150 Ligula

0
71

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo TANESCO SACCOS, kimekabidhi shuka 150 kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mtwara ya Ligula, zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.

Mjumbe wa TANESCO SACCOS, Mussa Chowo amesema mikakati ya chama hicho ni kuhakikisha kinagawa shuka katika hospitali zote za mikoa hapa nchini.

Uongozi wa hospitali hiyo ya Ligula umesema, shuka hizo zitasaidia kupunguza uhaba wa shuka uliopo hospitalini hapo.

Umesema kwa sasa baadhi ya vitanda havina shuka, na hivyo kuziomba taasisi nyingine kuisaidia hospitali hiyo.