Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara imenunua vifaa tiba na vifaa kinga vyenye thamani ya zaidi ya shillingi milioni 62 vitakavyosaidia kutumika endapo mtu mwenye maambukizi ya virusi vya corona atagundulika wilayani humo.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Dkt. Antipas Swai, mkuu wa wilaya hiyo, Sebastian Waryuba amesema vifaa hivyo vitaongeza ari kwa watumishi wa afya katika kuwahudumia wagonjwa wa Corona.
Kwa upande wake Dkt. Swai, amesema awali walikuwa na changamoto ya vifaa vya kuwakinga wauguzi na madokta, endapo mgonjwa wa Corona angebainika katika eneo hilo.
Vifaa hivyo vilivyonunuliwa ni pamoja na mashine mbili za kupumulia, barakoa (masks) na vipukusi (sanitizers).
Hapa chini ni picha zaidi zikiwaonesha viongozi wa wilaya hiyo wakikagua vifaa hivyo.