Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema kuwa ukaguzi wa anga uliofanywa leo asubuhi katika Mlima Kilimanjaro umebaini kuwa moto wote umedhibitiwa lakini vikosi vya askari vimetawanywa kwa ajili ya tahadhari.
Moto huo uliozuka Oktoba 11 mwaka huu umeathiri eneo la kilomita za mraba 95.5 ambazo ni sawa na 5% ya eneo lote la hifadhi lenye kilomita za mraba 1,700.
TANAPA imesema kuwa udhibiti wa moto huo umetokana na kazi kubwa inayoendelea kufanywa na askari, wananchi na Jeshi la Zimamoto.
Licha ya moto huo, shughuli za utalii katika Mlima Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida.