TAKWIMU ZA SEKTA YA MAWASILIANO TANZANIA

0
446

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameliambia bunge kuwa sekta ya mawasiliano imeendelea kukua, na kutaja takwimu za sekta hiyo kama ifutavyo;

  • Laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka 52,965,816 mwezi Aprili mwaka 2021 hadi kufikia laini 55,365,239 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 4.5.
  • Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.1 mwezi Aprili mwaka 2021 hadi kufikia milioni 29.9 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 2.7.
  • Watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka 27,326,938 mwezi Aprili mwaka 2021 hadi kufikia 35,749,298 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 30.8.
  • Watoa huduma wa Miundombinu ya mawasiliano wamefikia 23 ukilinganisha na watoa huduma 19 mwezi Aprili mwaka 2021 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.1.
  • Watoa huduma wa huduma za ziada (Application Services and Value Added Services) wamefikia 102 ukilinganisha na 13.

-Bei ya mwingiliano kati ya watoa huduma (Voice interconnection Charges) imeshuka kutoka shilingi 2.6 kwa dakika mwaka 2021 hadi shilingi 2.0 kwa dakika mwaka huu sawa na punguzo la asilimia 23.1.

  • Vituo vya kurusha matangazo ya redio vimeongezeka kutoka 200 mwaka 2021 hadi kufikia vituo 210 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 5 na vituo vya kurusha matangazo ya runinga vimeongezeka kutoka 50 mwaka 2021 na kufikia 56 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 12.
  • Cable Television zimeongezeka kutoka 40 mwezi Aprili mwaka 2021 na kufikia 59 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 47.5
  • Magazeti yameongezeka kutoka 272 na kufikia 284 mwezi Aprili mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 4.4.
  • Hadi Kufikia mwezi Aprili mwaka huu televisheni mtandao zimeongezeka kutoka 552 hadi 663 sawa na ongezeko la asilimia 20.1,
  • Blogu zimeongezeka kutoka 134 hadi 148 sawa na ongezeko la asilimia 10.4 na redio mtandao zimeongezeka kutoka 25 hadi 27 sawa na ongezeko la asilimia 8.0.

Akiwasilisha bajeti ya wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 bungeni jijini Dodoma waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya matumizi ya teknolojia za Utangazaji hasa maudhui mtandaoni ili kuongeza ajira kwa vijana.