Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi inatarajia kumfikisha mahakamani muda wowote kuanzia sasa hivi mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mtama, Suleiman Mathew.
Kamanda wa TAKUKURU mkoani humo, Stivine Chami akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari amesema mtuhumiwa anatuhumiwa kutoa rushwa ya shilingi milioni 1.5.
Mathew anatuhumiwa kutenda kosa hilo Agosti 24 mwaka huu kwa kutoa fedha hizo afisa uchaguzi wa Jimbo Mtama ikiwa ni fedha ya utangulizi kati ya shilling milioni 10 alizokuwa ameahidi kutoa kwa afisa uchaguzi pamoja na msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo.