TAKUKURU kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

0
664

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imesema kuwa itamuita kwa ajili ya mahijano Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kufuatia kutolewa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia John Mbungo amesema kuwa tayari wamewahoji viongozi wa chama hicho pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu, Dkt. Vicent Mashinji kufuatia kutolewa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za michango ya wananchama wa chama hicho na fedha za ruzuku.

“Freeman Mbowe ataitwa, kwa sababu sasa hivi ametuambia hayupo Dar es Salaam,” amesema Mbungo.

Amesema viongozi mbalimbali wa CHADEMA waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje, John Mrema, na baadhi ya wanachama.

Ameongeza kuwa suala hilo litachukua muda kwani wanashirikiana pia na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na tayari wamepata nyaraka mbalimbali wanazoendelea kuzifanyia kazi.