Tahadhari yatolewa Kimbunga Jobo kupiga Tanzania

0
140

Kimbunga hafifu kimeyapiga maeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi nchini Tanzania jana, kufuatia kujitokeza kwa mgandamizo wa hewa katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kimbunga hicho kinachojulikana kwa jina la Jobo kinatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo hususan katika maeneo ya mwambao wa pwani ya kusini, maeneo ya Lindi na Mtwara.

Samwel Mbuya ambaye ni Meneja wa Kituo kikuu cha utabiri TMA amesema kuwa, kimbunga Jobo kipo umbali wa takribani kilomita 930 kutoka pwani ya Lindi na takribani kilomita 1,030 pwani ya Mtwara.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imewataka Wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia mwelekeo wa upepo na mawimbi ya bahari katika maeneo husika.

Kimbunga hicho pia kilisafiri kwa kasi ya mwendo wa kilomita 1,022 Kaskazini mwa mji mkuu wa Madagascar – Antananarivo.