Tafiti kusaidia wafugaji

0
151

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki ametoa wito kwa taasisi zinazofanya tafiti nchini kutumia tafiti hizo kusaidia wananchi hasa wafugaji, ili waweze kuboresha shughuli zao za ufugaji.

Waziri Ndaki ameyasema hayo mkoani Mbeya wakati wa kikao jumuishi kilichokutanisha viongozi na wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali zinazoshiriki maonesho ya wakulima maarufu Nanenane kitaifa, yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale.

Ametaka tafiti zinazofanyika nchini matokeo yake yarudi kwa wananchi, ili wananchi hao hasa wafugaji wanufaike nazo badala ya kuzifungia.

Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi ameongeza kuwa kwa sasa kuna mwamko mkubwa kwa wananchi kufanya ufugaji wenye tija.

Hata hivyo amesema wafufaji bado wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji na kutokuwa na soko la uhakika la bidhaa za mifugo.