Tabora watakiwa kutunza mazingira

0
873

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  amesema kuwa serikali inaboresha na kujenga barabara mkoani Tabora, hivyo uboreshaji huo uendane na utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo mkoani Tabora wakati wa kongamano la mazingira lililolenga kujadili hali ya  mazingira ya mkoa huo, kongamano lililohudhuriwa na wadau wa mazingira kutoka taasisi mbalimbali.

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa wakati wa kongamano hilo ni kupunguza matumizi ya kuni katika kukaushia tumbaku, kwa kuwa matumizi ya kuni yamekua yakisababisha uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo.

Jingine ni kutunza miti iliyopandwa wakati wa kampeni iliyozinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, -Aggrey Mwanri,  ambapo miti ilipandwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Tabora, -Aggrey Mwanri amesema kuwa  mkoa huo unafanya jitihada kubwa katika kuhifadhi uoto wa asili pamoja na kupanda miti ili kukabiliana na hatari ya jangwa.