Tabora waanza kunufaika na mradi wa maji Ziwa Victoria

0
392

Baadhi ya wakazi wa wilaya za Nzega na Igunga mkoani Tabora wamesema kukamilika kwa mradi wa maji wa Ziwa Victoria kumesaidia kupungua kwa magonjwa ya Typhoid na kuhara, kwani hivi sasa wanapata maji safi na salama kupitia mradi huo.

Wakizungumza na TBC wakazi hao wamesema walikuwa wakitumia maji yasiyo salama kutoka katika madimbwi na visima huku wakitumia muda mrefu kusaka maji kuliko kuzalisha mali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Mazingira Igunga, Rapahel Milumba amesema wananchi wamepewa utaratibu wa kulipia kwa awamu ili waweze kumudu gharama za kuunganishiwa maji.

Serikali imetumia shilingi bilioni 600 kutekeleza mradi huu wa Ziwa Victoria katika wilaya za Nzega, Igunga, Uyui na Tabora.