Hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira iliyowasilishwa Bungeni Dodoma na Mwenyekiti wa kamati hiyo Jackson Gedion imesema taasisi za Serikali zinadaiwa malimbilizo ya madeni ya ankara za maji zinazotolewa na Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) ambapo hadi Desemba 31, 2023 taasisi hizo zimefikisha deni la jumla ya shilingi Bilioni 26.2.
Amesema kutolipwa kwa deni hilo kwa muda mrefu kunasababisha mamlaka hiyo kupungukiwa na uwezo wa kujiendesha hata kushindwa kuwahudumia Wananchi kwa wakati na kwa ufanisi.
Kufuatia hoja hiyo, Bunge limeazimia jambo hilo kushughulikiwa ili RUWASA iweze kujiendesha na kutoa huduma kwa Wananchi kama ilivyokusudiwa.