Sudan Kusini Yaonyesha nia ya Kuwekeza Tanzania

0
331

Sudan Kusini imeonyesha nia ya kutumia bandari za Tanzania na viwanja vya  ndege kupitisha mizigo inayosafirishwa kwenda katika nchi hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, waziri wa viwanda, biashara, uwekezaji na jumuiya ya Afrika Mashariki wa Sudan Kusini Paul Mayom Makech amesema nchi yake imepakana na nchi nyingi afrika zenye bahari na hivyo inaweza kuzitumia bandari za nchi hizo kupitishia mizigo.

Kwa upande wao Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Isack Kamwelwe wamesema uboreshaji wa miundombinu ya bandari  na viwanja vya ndege kutaboresha biashara kati ya Tanzania na Sudan Kusini.