Sudan Kusini kutumia bandari ya Dar es Salaam

0
148

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na Sudan Kusini kutumia bandari ya Dar es Salaam katika kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Albino Ayuel Aboug.
 
Ametoa ombi hilo baada ya kupokea ombi la Rais Salva Kiir ambaye ameomba Sudan Kusini itumie bandari ya Dar es Salaam katika kusafirisha mizigo yake.
 
Katika ujumbe wake pia Rais Kiir ametaka kuimarishwa kwa uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Sudan Kusini na kwamba pindi reli ya kisasa itakapokamilika Sudan Kusini  ingependa kusafirishia bidhaa zake kupitia reli hiyo.
 
Sudan Kusini imeongeza kuwa inahitaji kununua chakula kutoka Tanzania, na kupata walimu kutoka Tanzania ambao watafundisha lugha ya kiswahili kuanzia ngazi ya shule za msingi.