Suala la kina Mdee bado kizungumkuti

0
173

Chama cha Demoktrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewawekea pingamizi waliokuwa wanachama 19 wa chama hicho akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho Taifa BAWACHA Halima Mdee, katika maombi yao Mahakama Kuu kuizuia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwavua ubunge baada ya chama hicho kuwavua uanachama.
 
 
Pingamizi hilo la CHADEMA litasikilizwa tarehe 29 mwezi huu majira ya mchama Mahakamau Kuu.
 

Hata hivyo, Mahakama Kuu imetoa amri ya kuwa hadhi ya wabunge hao ibaki kama ilivyo mpaka siku ya usikilizwaji wa pingamizi hilo la CHADEMA.
 
Mdee na wenzake wamefungua maombi Mahakama Kuu dhidi ya bodi ya wadhamini wa CHADEMA wakiomba ridhaa ya kufungua shauri la kupinga kuvuliwa uanachama wa chama hicho.
 
Pamoja na maombi hayo ya ridhaa, pia wamefungua maombi ya amri ya zuio dhidi ya NEC na Spika kutochukua hatua dhidi ya uamuzi wa CHADEMA kuwavua uanachama.
 
Maombi hayo yaliyopangwa kusikilizwa na Jaji Mustapha Ismail hii leo, siku ambayo mawakili wa CHADEMA wameweka pingamizi dhidi ya maombi hayo ya zuio.