SSRA yaendelea kutoa ufafanuzi kuhusu mafao ya watumishi

0
1671

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt Irene Isaka amesema kuwa mkanganyiko unaotokea juu ya kanuni ya kukokotoa asilimia 25 ya mafao ya mkupuo kwa mtumishi baada ya kustaafu unatokana na lugha ya kitalaamu inayotumiwa kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kutoeleweka kwa haraka.

Akitoa ufafanuzi huo jijini Dar es salaam, Dkt ย Isaka amesema kuwa asilimia hiyo inatokana na mshahara wa mtumishi na siyo michango yake.

Kuhusu kipindi cha malipo kwa mtumishi aliyestaafu, Dkt Isaka amesema kuwa ย mtumishi huyo atalipwa mafao yake kwa muda wote wa maisha yake.

Siku za hivi karibuni, ย kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu kanuni maalumu inayotumika kukokotoa mafao ya wastaafu.