Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kutovaa tai nyekundu, wakati wa kikao cha saa 10:00 jioni, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge.
“Napenda kuwakumbusha waheshimiwa wabunge, siku anapokuja kiongozi mkuu wa nchi (bungeni), basi haishauriwi sana kuvaa tai nyekundu”. Amesema Spika
“Nadhani tunakubaliana, ile red inabakia na wenye mamlaka, kwa hiyo ni vizuri kuyajua haya mambo,baadae jioni tutakapo rudi, ukivaa tai nyekundu utarudia getini” amesema spika Ndugai.
Majira ya saa 10:00 jioni hii leo, Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kushika wadhifa huo Machi 19,2021.