SOS: Tupo tayari kujikinga na UVIKO-19

0
151

Mwinjilisti wa umoja wa wakristo wa SOS adventure kutoka nchini Sweden Johannes Amritzer amesema wapo tayari kufuata maelekezo ya wataalam wa afya katika kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa UVICO-19 kwenye mkutano wa dini unaotarajia kufanyika katika viwanja ya Usagara, Tanga.

Amritizer ametoa kauli hiyo wakati alipokua akizungumza na wanahabari jijini Tanga. Amesema mkutano huo unaotarajia kukutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania utafuata taratibu zote za afya ikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.

Mbali na kufanyika kwa mahubiri hayo pia amesema watatoa misaada mbalimbali kwa jamii,ikiwemo kugawa tisheti, taulo za kike pamoja na vifaa vya michezo kwa watoto.

Mkutano huo unatarajia kudumu kwa muda wa siku tano utaanza Agosti 4 mpaka Agosti 8.