Wizara ya Ujenzi na timu ya wataalam kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakishirikiana na makandarasi, wanaendelea na zoezi la urejeshaji wa miundombinu ya barabara katika eneo la Songas ambalo nalo lilikatika katika Barabara Kuu ya Lindi – Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.
Hadi kufikia leo kazi ya urejeshaji wa miundombinu ya barabara katika eneo la Somanga ipo katika hatua za ukamilishaji ambapo magari ya mawe yameruhusiwa kupita kuelekea maeneo mengine yaliyoathiriwa.