Soko kubwa la Mitumba lililopo Manispaa ya Kigoma – Ujiji limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Februari 10, 2024.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Kigoma kwa kushirikiana na Wananchi wamefanikiwa kuzima moto huo huku chanzo halisi cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.