Mkutano mkuu wa chama cha Skauti Tanzania unataŕajiwa kufanyika Julai 2 mwaka huu jijini Dodoma.
Rais wa Skauti Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amesema pamoja na kuwa agenda kuu ya mkutano huo ni uchaguzi, pia kutakuwa na majadiliano mengine kuhusu chama hicho.
Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ametangaza tarehe ya mkutano huo Mkuu wa Skauti alipofanya mazungumzo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Muhamed.
Kwa upande wake waziri huyo wa Elimu Zanzibar Lela Musa amesema katika mkutano mkuu wa chama hicho cha Skauti Tanzania
kutajadiliwa suala la ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya Skauti ili iwekwe sawa katika katiba ya sasa ya chama hicho.