Singida BS kushiriki mashindano ya kimataifa Afrika

0
163

Singida Big Stars itashiriki mashindano ya kimataifa ya Afrika, uwezekano mkubwa ukiwa ni Kombe la Shirikisho Afrika, msimu ujao ikiwa na uhakika wa kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.

Hadi sasa vijana hao wa Liti, Singida wana alama 51 ambazo haziwezi kufikiwa na Namungo FC au Geita Gold FC, na hivyo kuiweka Singida BS ikiwa nafasi ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu.

Timu hiyo inaingia kwenye rekodi za timu nyingine ambazo zilipanda daraja na msimu uliofuta kucheza michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Namungo, KMC na Geita Gold zimewahi kupanda daraja na kucheza michuano hiyo