Simba SC imeitandika Biashara United bao moja kwa bila katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa karume mkoani Mara
Bao pekee la Simba limefungwa na Bernard Morrison na kuipa Simba alama 3 muhimu huku ikifikisha jumla ya alama 42 katika msimamo wa ligi hiyo
Simba hadi sasa imecheza mechi 18 ikiwa na michezo miwili mikononi huku Yanga ikiongoza ligi hiyo ikiwa na alama 46 baada ya kucheza mechi 20