Mechi ya kirafiki kati ya wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) waliojigawa kama Yanga na Simba imemalizika kwa sare ya mabao 3-3 katika uwanja wa chuo cha Ustawi Jijini Dar es salaam
Yanga walitoka kifua mbele kipindi cha kwanza kwa kupata ushindi wa magoli 3, lakini kipindi cha pili Simba walirudi na nguvu zaidi na kusawazisha magoli hayo na kufanya ubao usomeke 3-3 hadi dakika 90 za mchezo