Simba Queens watashuka katika dimba la Prince Moulay Al Hassan mjini Rabat nchini Morocco hii leo kusaka nafasi ya tatu katika ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa wanawake kwa kuumana na Mabingwa wa Nigeria, Bayelsa Queens.
Simba Queens iliondoshwa katika nusu fainali ya michuano hiyo msimu huu na Mabingwa watetezi Mamelod Sundown huku Bayelsa wakiondoshwa na wenyeji ASFAR Club.
Endapo Simba Queens itashinda katika mchezo huo wa saa 4 usiku wataweka historia ya kushiriki kwa mara ya kwanza na kumaliza katika nafasi tatu za juu na watatunukiwa medali ya shaba.