Simba na Yanga kukutana Nusu Fainali ASFC

0
208

Watani wa jadi Simba na Yanga huenda wakakutana katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho ya Azam (ASFC) endapo watashinda michezo yao ya robo fainali ya michuano hiyo kufuatia droo iliyochezeshwa leo.

Katika droo iliyopangwa hii leo kuelekea robo fainali, Yanga watakutana na Geita Gold Fc, Simba watakutana na Pamba FC ya Mwanza, Kagera Sugar kuvaana na Coastal Union na Azam watakutana na Polisi Tanzania.

Kwa mujibu wa TFF nusu fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza na Arusha