Simamieni majukumu ipasavyo

0
258

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewataka watendaji wa ngazi zote serikalini kusimamia kikamilifu majukumu yao ili kujenga uchumi imara kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye eneo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji jijini Tanga katika mtambo wa kutibu na kuzalisha maji Mowe. Huduma za maji Tanga zinatazamiwa kuboreka maradufu kupitia Hati Fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji iliyozinduliwa leo.

Amesema mkoa wa Tanga ni mkoa wa sita katika kuchangia pato la taifa, hivyo serikali inauona kama moja ya mikoa ya kimkakati. Ni katika muktadha huo ameomba mshikamano uliopo uendelee.