Siku ya Ukimwi Duniani yaadhimishwa leo

0
75

Tanzania leo inaungana na mataifa mbalimbali duniani, kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani.

Siku ya Ukimwi Duniani huadhimishwa Desemba Mosi kila mwaka, ambapo wadau mbalimbali wanapata fursa ya kujadili na kutathimini mikakati waliojiwekea katika mapambano dhidi ya Ukimwi.

Kitaifa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kinafanyika mkoani Lindi na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Tanzania inaadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani huku ikielezwa kuwa
imeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 62 toka mwaka 2020.

Hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi bado yapo kwa kiwango cha juu kwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 na hivyo kulifanya kundi hilo kuwa kwenye hatari zaidi.