Leo ni siku ya Afya Duniani ambapo Serikali za nchi mbalimbali duniani kwa kushirikiana na Wadau wa afya wanajadili mafanikio pamoja na changamoto zilizopo kwenye sekta hiyo.
Ujumbe wa Siku ya Afya Duniani kwa mwaka huu ni ‘Dunia yetu, Afya Yetu’.
Kwa mujibu wa wizara ya Afya ya Tanzania, ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Afya Duniani unawakumbusha Wananchi kuendelea kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kuhifadhi mazingira, kulinda vyanzo vya maji na kupanda miti.
Imesema hatua hizo zitachangia kupunguza hewa ya ukaa na kuilinda dunia ili iwe mahali salama pa kuishi.