Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema kuwa utaratibu wa kuwapata wagombea wa Urais umefuata taratibu zote zilizotakiwa.
Rais Shein ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akitoa salamu zake wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM.
Amesema kuwa katika mchakato huo wa kutafuta wanaowania Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM hakukuwa na upendeleo wowote na wote waliopita katika mchakato huo ilikuwa ni haki yao.
Rais Shein amesisiza kuwa, binafsi hajawahi kuwa upande wa mgombea yoyote kama ambavyo imekuwa ikisemwa na baadhi ya watu.
Kwa mujibu wa Rais Shein, Zanzibar itapata ushindi wa kishindo katika kinyang’anyiro cha Urais na ushindi huo utapatikana katika mazingira ya haki, amani na utulivu.