Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Carolyne Nombo, wametembelea baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hususani kujionea hali ya shule mbalimbali zilivyo.
Kutokana na hilo, wakiwa Rufiji mkoani Pwani, viongozi hao wamesema shule zote zilizoathiriwa na mafuriko nchini zitaboreshewa miundombinu au kujengwa upya katika maeneo salama kulingana na miongozo na nyingine kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Pichani, Profesa Mkenda (mbele kulia) na Profesa Carolyne Nombo (katikati ya mitumbwi) wakiendelea kukagua hali ya miundombinu ya elimu iliyoathirika katika eneo la Muhoro, Rufiji.
Wametoa wito wa wanafunzi kupokelewa katika shule za jirani zilizo salama wakati utaratibu wa kuzikagua na kuzifanyia tathmini shule zilizoathirika ukiendelea.