Shule ya msingi ilipoanzia safari ya kielimu ya Rais Mkapa

0
220

Hii ni Shule ya Msingi Lupaso, sehemu ambayo safari ya kutafuta maarifa ya Marehemu Rais Benjamin Mkapa ilianzia mwaka 1945.

Shule hii iliweka msingi imara na kumuwezesha kupita katika taasisi nyingine za elimu na kumuwezesha kukabidhiwa fungua za Ikulu ya Tanzania mwaka 1995, nafasi aliyoitumikia hadi mwaka 2005.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Charles Maduka amesema serikali imewapa shilingi milioni 400 kwa ajili kujenga shule, na walipanga kumualika Rais Mkapa kuja kuizindua.

Ameongeza kuwa kiongozi huyo alikuwa na mchango mkubwa katika elimu na kwa kutambua hilo eneo la darasa alimosoma kiongozi huyo patajengwa maktaba.

Kwa upande wake Mwalimu Tusuwege Kayinga amesema atamkumbuka Rais Mkapa kwa namna alivyowasaidia wafanyakazi kupata mikopo yenye riba nafuu ambayo amenufaika nayo.