Shule ya Kimange yapatiwa vitabu

0
219

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kimange iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamepokea msaada wa vitabu vya zaidi ya shilingi milioni 4 kutoka kwa wadau wa elimu ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu shuleni hapo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo mdau wa elimu kijijini hapo, Juma Gurumo amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha watoto kusoma bila msongamano uliokuwepo awali.

Akipokea vitabu hivyo Mkuu wa Shule, Kimange Mmbwana amesema awali kitabu kimoja kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi nane kwa wakati moja.

Vitabu vilivyotolewa shuleni hapo ni vya mchepuo wa sayansi, sanaa, kiingereza na hisabati.