“Shikamoo wabunge” yatumika kusalimu wabunge

0
104

Mgombea nafasi ya ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Hasnuu Makame amewavunja mbavu wabunge baada ya kuanza kuomba kura kwa kuwasalimia wabunge “shikamoo”.

Licha ya Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kuwataka wagombea wa nafasi hiyo kujieleza kwa kutumia lugha ya kiingereza, lakini Dkt. Makame aliomba kutumia kiswahili na kuwasalimia wabunge “Shikamooni Wabunge”.

Baada ya salamu hiyo wabunge waliangua vicheko kutokana na rika ya mgombea huyo na mtindo “style” aliyotumia kuombea kura.

Uchaguzi wa wawakilishi tisa wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki umefanyika hii leo ambapo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepiga kura kuwachagua wawakilisi hao.