Shigella kushughulika na kero za Ulanga

0
169

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Martine Shigella amesema atahakikisha anapita kwenye vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Ulanga, ili kusikiliza na kutatua kero zote zinazowakabili Wananchi wa vijiji hivyo.

Shigella ameyasema hayo kwenye Baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Ulanga, ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya ziara wilayani humo tangu ahamishiwe mkoani Morogoro akitokea mkoani Tanga.

Amesema atahakikisha kero za Wananchi wa Ulanga zinatatuliwa kwa haraka, ili kuwawezesha Wananchi hao kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali.