Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Aboubakar Kunenge amepiga marufuku sherehe zote mkoani humo katika kipindi chote cha siku 21 ambazo Taifa litakuwa likiomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli.
Kunenge ametoa agizo hilo wakati wa mkutano.wake na Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam.
Amesema Watanzania kwa sasa wapo katika majonzi makubwa ya kuondokewa na kiongozi wao, hivyo si uungwana kwa wengine kuendelea na sherehe katika kipindi cha maombolezo.
Dkt John Magufuli ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61 atazikwa tarehe 25 mwezi huu wilayani Chato mkoani.Geita, ambapo kwa mkoa.wa Dar es salaam Wakazi wake wtatoa heshima zao za mwisho Tarehe 21 siku ya Jumapili.