Shauri la kina Mdee kusikilizwa leo

0
215

Shauri la waliokuwa wanachama 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaoomba ridhaa ya mahakama kufungua shauri la kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama linaanza kusikilizwa mchana huu na Jaji Mustapha Ismail.
 
Juni 23 mwaka huu wanachama hao ambao ni pamoja na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho Taifa BAWACHA Halima Mdee, walifungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya CHADEMA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Hii ni mara ya pili Mdee na wenzake kufungua shauri hilo baada ya maombi yao ya awali kutupwa na mahakama hiyo, kutokana na kasoro za kisheria.