Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi, amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Mhandisi Zena Said imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza hii leo.
Dkt Mwinyi amefanya uteuzi huo kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na Chama cha ACT Wazalendo.
Sherehe ya kumuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar itafanyika hapo kesho saa nne asubuhi, Ikulu Zanzibar.