Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo
Shaka ametoa pongezi hizo wakati wa kongamano maalum la kumpomgeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania lililoandaliwa na Jukwaa Jamii Mpya .
“Rais Samia amezitembelea nchi takribani 22, kwa zaidi ya awamu 25 nchi yetu imeendelea kufunguka kiuchumi kupitia biashara na nchi za nje. Takwimu za hivi karibuni zimerekodi ongezeko kubwa la mauzo ya nje kwa bidhaa na huduma za Tanzania katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki.” amesema Shaka
Ameongeza kuwa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya nchini Kenya zimeonesha kukua maradufu kwa mauzo ya Tanzania katika nchi hiyo kwa takribani shilingi bilioni 20.5 kwa nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 kutoka shilingi bilioni 10.8 kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.