Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndungulile amesema lengo la Serikali kuondoa kodi katika simu, Vishikwambi (Tablets) na Modem ni kuongeza watumiaji wa teknolojia ya habari nchini mpaka kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.
Dkt. Ndungulile pia amewatoa hofu Watanzania kuhusu tozo zilizopendekezwa za umiliki wa laini za simu na miamala na kusema kuwa zina lenga katika kukuza sekta hiyo na sekta nyingine hapa nchini.
Amesisitiza kuwa ukuaji wa teknolojia ya habari unatoa fursa za ukuaji wa uchumi, hivyo Serikali imeamua kuondoa kodi kwenye simu za mkononi, Vishikwambi (tablets) na modem ili kuwawezesha Watanzania kunufaika na ukuaji wa teknolojia