Serikali yatoa onyo kwa wakandarasi watakao hujumu kiwanda cha sukari

0
295

Waziri Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda amesema serikali haitakuwa na mzaha na wakandarasi watakao bainika kuhujumu mradi wa ujenzi wa kiwanda cha  Sukari cha Mkulazi  kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Waziri Kakunda amesema hayo wilayani kilosa baada ya kutembelea maendeleo ya kiwanda hicho na kusisitiza wakandarasi ambao watapewa zabuni  ya kulima mashamba hayo kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kazi hiyo iweze kukamilika kwa wakati .

Hapa Waziri Kakunda anaeleza msimamo wa serikali katika kuhakikisha kazi zote zinazoendelea kufanywa katika eneo hilo zinakamilika kwa wakati ili kiwanda hicho kiweze kufunguliwa ifikapo disemba mwaka huu.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba amesema Serikali inaweka mikakati ya  kuhakikisha wakulima wa nje wananufaika kupitia kiwanda hicho.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi  Dokta Elidalita Msita akaeleza changamoto mbalimbali zilizosababisha kusuasua kwa ujenzi huo na mikakati ya kukabiliana nazo.