Serikali yateta na wasafirishaji mizigo

0
139

Serikali kupitia kwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji imefanya mazungumzo na ujumbe wa kampuni ya APM ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Kanda ya Afrika na Ulaya Igor Van Den Essen, ambapo wamejadili masuala ya kibiashara hususani sekta ya usafirishaji.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Kigali, Rwanda, Waziri Kijaji amemhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Tanzania iko tayari kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo na amemkaribisha mwekezaji huyo kuja Tanzania ili kujadili fursa zaidi za kiuwekezaji.

Kampuni ya APM ndiyo inasimamia shughuli ya kampuni ya usafirishaji mizigo ya Maersk.