Serikali yataka tafiti kubaini maeneo yenye maji

0
162

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua visima vya dharura vinavyosafishwa, kufufuliwa na kuunganishwa katika mfumo wa usambazaji maji kwa wananchi na kuagiza zoezi hilo pamoja na uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali liwe endelevu.

Waziri Mkuu amekagua
visima hivyo katika eneo la Tabata Relini na Mwananyamala Komakoma mkoani Dar es Salaam, ambapo pia ameshuhudia usafishwaji wa kisima pamoja na zoezi la usambazaji maji.

Visima hivyo ni miongozi mwa visima 197 vilivyochimbwa na serikali mkoani Dar es Salaam ambapo kwa sasa 160 vimefufuliwa na kutoa lita milioni 29.4 za maji kwa siku.

Waziri Mkuu Majaliwa ameuagiza uongozi wa bonde la Wami Ruvu pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuendelea kufanya tafiti kubaini maeneo yenye maji mengi na kuchimba visima na kuyaingiza katika mfumo.