Serikali yasisitiza kuondolewa kwa michango isiyo ya lazima shuleni

0
400
Waziri mkuu amewataka wazazi na walezi wote nchini kushiriki kikamilifu katika kufuatilia mienendo ya watoto wao shuleni.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa shule zote zinazomilikiwa na serikali kuhakikisha wanaendelea kutekeleza agizo la kudhibiti michango isiyo ya lazima kwenye shule zao. 

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo mkoani Lindi, wakati akizungumza na wadau wa elimu wilayani Ruangwa.

Amesema lengo la serikali la kutoa elimu bila malipo ni kuhakikisha watoto wote hasa wale wanaotoka katika familia zisizokuwa na uwezo kupata fursa ya kusoma, hivyo wasitozwe michango mingine isiyo ya lazima.

Waziri mkuu pia amewataka wazazi na walezi wote nchini kushiriki kikamilifu katika kufuatilia mienendo ya watoto wao shuleni na kuhakikisha wanakwenda shule badala ya kuliacha jukumu hilo kwa walimu pekee.