Serikali yaongeza muda wa maombi ya ajira za ualimu

0
483

Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeongeza muda wa kupokea maombi ya nafasi za ajira ya walimu wa Shule za Msingi na Shule
za Sekondari na mafundi sanifu wa maabara za Shule za Sekondari kutoka Septemba 21, 2020 hadi Septemba 30, 2020.

TAMISEMI imechukua hatua hiyo baada ya kupokea maoni ya wadau juu ya uwepo wa changamoto za upatikanaji wa mtandao zilizojitokeza mara baada ya mfumo wa kupokea maombi ya ajira ya walimu kufunguliwa rasmi Septemba 7, 2020.

Waombaji wenye sifa wametakiwa kuendelea kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha https://ajira.tamisemi.go.tz (Online Teacher Employment Application System – OTEAS).