Serikali yaombwa kutoa muda wa kutumika sheria mpya ya uzito wa malori

0
359

Chama cha Wasafirishaji Tanzania kimeiomba serikali kuongeza muda zaidi wa kuanza kutumika sheria mpya ya uzito wa malori ya Afrika Mashariki iliyoanza Januari Mosi mwaka huu ili kumaliza changamoto zinazojitokeza ikiwemo kukwama kwa magari katika mpaka wa Tunduma.

Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania Omary Kiponza amesema sheria hiyo inakinzana na ile ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika Sadc kwani tayari kuna mizigo iliyopakiwa kuja Tanzania imekwama mpakani na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara na kuathiri uchumi wa bandari za Tanzania.

Akijibu hoja hizo kwa njia ya simu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema walitoa muda wa miezi sita kwa wadau wa usafirishaji kupitia sheria hiyo kabla ya kuanza utekelezaji wake..

Sheria ya uzito wa malori ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanza kutumika Januari Mosi mwaka huu lengo likiwa ni kulinda miundombinu ya barabara.