Serikali yakukusanya zaidi ya shilingi Bilioni 48+

0
177

Serikali imekusanya zaidi ya shilingi Bilioni arobaini na nane tangu ianze kukusanya kodi kutoka kwenye miamala ya simu nchini hayo yamethibitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam


“Tangu makato ya tozo yaanze kwa hizi wiki 4 hadi leo tumekusanya zaidi ya shilingi bilioni 48. Zaidi ya bilioni 22 tulishapeleka kwenye maeneo ambayo hayana vituo vya afya (zaidi ya vituo 90), leo tumepeleka zaidi ya bilioni 15 kwenye eneo hilo hilo na kufanya vituo kuwa zaidi ya 150.


Zaidi ya bilioni 7 zimepelekwa kwenye madarasa, mtaona wenyewe tumepeleka fedha zijenge vituo 150 ambavyo vinaokoa maisha yetu, pia madarasa zaidi ya 500, ni watoto wetu wanasoma.” Dkt. Mwigulu Nchemba

Pia Waziri Mipango amesema kati ya fedha hizo shilingi bilioni ishirini na mbili zimepelekwa kwenye vituo vya afya tisini kwajili ya mendeleo.
Na kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema tayari wameshapatiwa fedha hizo ambazo zinakwenda kujengwa vituo vya afya miambili na saba kwenye tarafa ambazo hakuna vituo hivyo.

Waziri Mwigulu amewaomba watanzania kuiunga mkono serikali katika suala hili kwakuwa lengo la serikali kuboresha maisha ya kila mtanzania kwa kuhakikisha miradi ya maendeleo inafanikiwa.

“Fedha ni zetu, maisha ni yetu na serikali ni yetu tuunge mkono” Dkt. Mwigulu Nchemba