Serikali yafuta tozo ya miamala ya Kibenki

0
162

Serikali imefuta tozo kwenye miamala ya kutoa na kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za benki kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akitoa taarifa za mawaziri kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Mwigulu amesema serikali imefuta tozo za miamala ya benki kwenda kwenye mitandao ya simu kuanzia tarehe 01, Oktoba 2022.

Pia serikali imefuta tozo kwenye miamala ya kutuma pesa kutoka Benki A kwenda Benki B.

Serikali imefuta tozo za miamala kutoka kwenye mitandao ya simu kwenda akaunti za benki na pia imefuta tozo kwenye miamala ya kutoa fedha kwenye ATM ama wakala wa benki.

Serikali pia imebadili utaratibu wa kukusanya kodi ya zuio ya pango ambapo badala ya kukusanywa na wapangaji sasa itakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Waziri Mwigulu amesema, baada ya kufutwa kwa tozo hizo, serikali itabana matumzi kwenye maeneo mbalimbali ili kufidia fedha ambazo zingekusanywa kupitia tozo ambazo zimefutwa.