Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli amewaahidi wakazi wa kata ya Kasharunga wilayani Muleba, Kagera kuwa atashughulikia changamoto ya maji na ongezeko la tozo kwa wavuvi.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni Dkt. Magufuli amesema Serikali ya CCM imetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 500, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na ukarabati wa kivuko cha MV Victoria.
Dkt. Magufuli amewaomba wananchi hao kuwachagua madiwani, wabunge na rais kutoka CCM ili kutatua changamoto zilizobaki katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi,umeme, elimu na maji.
Dkt.Magufuli yupo Mkoani Kagera akiendelea na kampeni za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania