Serikali na taasisi za dini kuendelea kushirikiana

0
147

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene
amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini nchini ili kuhakikisha zinatoa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo Zanzibar wakati wa Ibada Kuu ya Upatanisho iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Zanzibar, Kanisa Kuu la Kristo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Amewaomba viongozi wa dini kusisitiza suala la kulinda umoja. amani na mshikamano kwani umoja ni muhimu katika ujenzi wa Taifa.

Aidha, Waziri Simbachawene ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia sera yake ya R4, zikiwa na maana ya maridhiano, upatanisho, mageuzi na ustahimilivu, ni vema Watanzania wakaijenga upya nchi yao kupitia Ibada hiyo.